
Mkopo wa elimu ya juu unaombwaje?
Maombi yote yanafanywa kwa njia ya mtandao wa Bodi ya Mikopo
Kila mwombaji anapaswa kusoma kwa makini mwongozo unaotolewa ndani ya mwaka husika wa masomo
Mwombaji atumie namba ya mtihani wa kidato cha nne kujisajili
Hali ya Kijamii na Kiuchumi (Zinazoongeza Kipaumbele)
Waombaji wenye hali zifuatazo hupewa kipaumbele zaidi katika upangaji wa mikopo:
Hali ya Kijamii na Kiuchumi (Zinazoongeza Kipaumbele)
Sifa za Msingi za Kupata Mkopo wa Diploma HESLB 2025/2026
Ili kustahili mkopo wa diploma, lazima ukidhi vigezo vifuatavyo:
Uwe raia wa Tanzania na usizidi umri wa miaka 35 wakati wa kuomba.
Uwe umepata admission kamili (full-time) katika chuo kinachotambulika na TCU au NACTVET kinachotoa kozi ya diploma.
Usiwe na ajira rasmi au mkataba wa kudumu katika sekta yoyote.
Uwe umemaliza CSEE (Form Four), Cheti, au ACSEE ndani ya miaka 5 iliyopita (2021–2025).
Uwe na maombi kamili na sahihi kupitia mfumo wa OLAMS (Online Loan Application and Management System).
Kwa wanafunzi wanaoendelea (continuing students), lazima wawe wamefaulu mitihani ya mwaka uliopita na kuwasilisha matokeo kupitia chuo chao.
Waombaji wenye hali zifuatazo hupewa kipaumbele zaidi katika upangaji wa mikopo:
- Uyatima: Aliyefiwa na mzazi mmoja au wazazi wote wawili.
- Kaya Duni (TASAF): Familia inayofadhiliwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) au taasisi nyingine za kitaifa zinazotoa ufadhili kwa kaya zenye vipato duni.
- Ulemavu: Mwombaji mwenye ulemavu wa mwili, au mzazi/mlezi wake mwenye ulemavu.