UCHAMBUZI WA DIWANI YA FUNGATE YA UHURU

wazaelimu

Administrator
Staff member
Jun 15, 2026
47
0
6
Screenshot 2026-06-18 204234.png


KITABU: FUNGATE YA UHURU

MWANDISHI: MOHAMED S. KHATIBU

WACHAPISHAJI: DUP

MWAKA: 1988

UTANGULIZI


Fungate ni kipindi cha siku saba baada ya harusi..Ni kipindi ambacho Bwana na bibi harusi hula na kunywa tena milo ya kuchagua wakati wote wa fungate.Fedha na vifaa vitumiwavyo na maharusi huwa ni vya kuazima au kuchangiwa(si lazima viwe vyao) Wanapewa kutoka kwa ndugu na jamaa na hata na vijana wa kuwahudumia.Wachangaji hufanya hivyo kwa sababu wanajua kuwa fungate ni ya muda mfupi(siku saba tu),hivyo huvumilia.

Fungate ni lazima iwe na kikomo.Ikizidisha kikomo hicho ibadili jina labda iitwe unyang’anyi,ulimbwende,uvivu,uzembe au jina lolote lenye kashfa hasa unafiki au usaliti.Mwandishi wa diwani hii ameimwaga ghadhabu hiyo kwa hao maharusi waliohesabu ukarimu wao kuwa ni upumbavu.

Uhuru:Uhuru ni neno linalopendwa sana na wanasiasa wa ubepari au ujamaa.Hekaheka za uhuru(kudai,kuomba au kupigania) zinaweza kufananishwa na shughuli za kutafuta mchumba,kupeleka posa kulipa mahari,na kufunga ndoa.

Katika kipindi chote cha uhuru, watu, hususani viongozi,hufurahi na kufanya sherehe ambazo huwagharimu raia-mali na vitu mbalimbali.Lakini kwa kuwa uhuru ni kitu cha thamani kama maharusi,raia hukubali kugharimia sherehe hizo.Lakini pia sherehe za uhuru kama fungate hutazamiwa iwe ya muda mfupi –labda mwezi mmoja au miwili.

Raia wanchi zilizopata uhuru barani Afrika walikuwa na shauku ya kupata maendeleo lakini hawajafikia lengo lao hadi sasa kwa sababu viongozi wetu wanaendeleza Fungate ya Uhuru.Hivyo viongozi wanchi za Afrika wamewasaliti wananchi wao waliowachagua.Katika utangulizi mwandishi anasema ;

Nikate tama,

Kwani tuendavyo,hatufiki,

Vile ipasavyo,hayakamiliki,

Mambo yalivyo,ni unafiki,

Tumesalitiwa!


MAUDHUI

Fungate ya Uhuru ni diwani inayojdili kwa mapana sana juu ya matatizo mbalimbali yanayokwamisha ujenzi wa jamii mpya hapa Tanzania.Matatizo hayo ni kama vile usaliti,unafiki,wizi,hujuma,udanganyifu,rushwa pamoja na uongozi mbaya.

Dhamira Kuu: Ujenzi wa jamii mpya.

Mwandishi anajadili kwa kiasi kikubwa suala la ujenzi wa jamii mpya.Mwandishi anaitaka jamii itupilie mbali unyonyaji , uonevu, dhuruma, udanganyifu, wizi, unafiki, umasikini, uongozi mbaya na ukandamizaji wa watu wa tabaka la chini ili kuijenga jamii kwa upya.Jamii ambayo hatamu zote za uongozi (utawala,siasa na uchumi) zitakuwa mikononi mwa wakulima na wafanyakazi kwa misingi ya haki na usawa.

Itikadi ya kujenga jamii mpya ilijengeka juu ya siasa ya ujamaa na kujitegemea ambayo ilitangazwa mwaka 1967 baada ya kutangazwa kwa Azimio la Arusha.Hadi 1988,mwandishi anaandika kitabu hiki anaonesha kuwa bado hatujafanikiwa kujenga jamii mpya hapa Tanzania.Hii inatokana na sababu zifuatazo;

Kwanza,bado kuna dhuruma, usaliti,unyonyaji na wizi wa mali za umma.katika shairi la “Wingu’’ mwandishi anasema;

Bado:

Wingu limetanda,

Limetanda,

Na kutughubika ghubi,

Mvua:

Lakini hainyeshi,

Hainyeshi,

Ukame umetanda waa!

Mimea:

Tulipanda kwa miongo,

Kwa miongo,

Yote imekauka!


Pia katika shairi la “Wizi”mwandishi ameonesha dhahiri kuwa wizi umo ikuluni, bomani, kanisani, misikitini, na hekaluni.Mwandishi ameonesha kuwa dini zawabariki wezi, polisi hulinda wezi, na majeshi huhalalisha wizi.katika ubeti wa 1 mwandishi anasema;

Wizi umo;

Kanisani,

Msikitini,

Kasirini,

Na bomani,

Wanyang’anywao ni waumini.

Pili, mwandishi ameonesha kuwa bado kuna matabaka katika jamii zetu.Ameonesha kuwa kuna tabaka la wenye nacho na tabaka la wasionacho.Tabaka la juu (utawala) unaolinyonya tabaka la chini(tawaliwa).Mfano katika shairi la “Fungate” mwandishi ameonesha jinsi tabaka tawala linavyofurahia maisha kwa kuishi katika majumba mazuri, kutembelea magari ya faharin, n.k.

Katika shairi la”Waja wa Mungu”mwandishi anaonesha jinsi tabaka la chini linavyoishi kwa shida.Kwa mfano, kula kwa shida, kulala kwa shida, kuvaa kwa shida, hawapati elimu na huduma nzuri za afya.

Tatu, mwandishi ameonesha kuwa, bado kuna uongozi mbovu katika jamii zetu.Mfano katika shairi la “Viongozi wa Afrika” mwandishi anashutumu vikali viongozi wanaotumia madaraka yao vibaya na kugandamiza watawaliwa.Anasema;

Viongozi wa Afrika,

Wanaotawala kwa mabavu,

Kujifanya ni washupavu,

Wao wachache na werevu,

Na umma wote ni mpumbavu,

Wanafiki,

Wazandiki”.


Pia shairi la “Njama” mwandishi anaonesha jinsi viongozi wanavyotumia njama mbalimbali kulinyonya tabaka tawaliwa.Viongozi wanatumia njama mbalimbali ili kuhakikisha kuwa hakuna anayewapinga wala kuhoji hata kidogo.

Nne, mwandishi anaonesha kuwa, kuna unyonyaji wanaofanyiwa wakulima katika kuuza mazao yao.Ameonesha kuwa wakulima hunyonywa na kudhurumiwa na kupewa bei kidogo wakati kuuza mazao yao.Shairi la “Naona”mwandishi linadhihirisha haya katika ubeti wa 6,ansema;